Mwimbaji wa nyimbo za dansi Christian Bella ameendelea kujiongeza kimuziki ili sauti yake adimu ifike kwenye kiwango cha kimataifa anachostahili.

Kiongozi huyo wa Malaika Band amesema kuwa amemshirikisha Koffi Olomide kwenye wimbo mmoja alipoenda kufanya ziara yake ya kimuziki nyumbani kwao DRC Kongo wiki iliyopita ambapo lengo lilikuwa kuitangaza ‘Amerudi’.

Hata hivyo, Bella ameeleza kuwa jina la wimbo huo ambao wameuimba kwa kuchanganya Kiswahili na Kilingala bado halijapatikana.

“Jina la wimbo litapatikana hivi karibuni kwa sababu ni kawaida yangu kuandaa nyimbo na kuzirekodi bila kuzipa majina ili kwanza mashabiki nao wasaidie kutoa jina ambalo wanaamini ni zuri,” alisema.

 

Ali Kiba Anaamini Pesa Imetumika Kumhujumu Tuzo Za AFRIMMA
CCM Wamchagua Job Ndugai Uspika Bunge La 11