Ali Kiba hajaridhika na matokeo ya tuzo za Afrimma zilizotolewa jana jijini Lagos na anaamini kuwa pesa ilitumika kumhujumu ili asiondoke na tuzo.

‘King Kiba’ ambaye alitajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele vitano hakuambulia kitu, na leo amendika kwenye mtandao wa Instagram kuwashukuru mashabiki wake na kueleza kile anachokiamini.

Ali Kibaa

“Asanteni Sana Najua Mmepiga Kura Sana Lakini Nilikuja Kugundua Baada Yakufatilia Kuwa Kuna Mambo Yanaendelea Ya Watu Wana Diriki Hata Kupoteza Pesa Zao Kwaajili Yangu Ila Nawaomba Fans Msinielewe Vibaya I will Always Be There For You #HapaKaziTu #KingKiba,” ameandika.

Diamond Platinumz alishinda tuzo tatu huku Vanessa Mdee akiondoka na tuzo moja hivyo kuifanya Tanzania kumiliki tuzo nne za Afrimma 2015.

Picha: Ronda Rousey Apigwa Vibaya Na Holly Holm Na Kuvuruga Rekodi Yake
Christian Bella afanya Collabo na Koffi Olomide