Mwanamke mbabe na bingwa asiyepigika, Ronda Rousey wikendi iliyopita alipoteza sifa hizo baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa Holly Holm katika pambano la “UFC Women’s Bantamweight Champion” la mapigano ya ‘Makonde na mateke’ (Martial Art/Kick Boxing) lililofanyika Marekani.

Rousey R

Rousey alianza kumkimbiza Holm ulingoni katika mzunguko wa kwanza huku akionekana kumvizia kwa hamu ya kutaka kumaliza pambano hilo ndani ya sekunde 48 kama alivyokuwa ameahidi, lakini mambo yalikuwa magumu.

Holm alimvizia sekunde ya 59 ya mzunguko wa pili na kumchapa konde lenye ujazo wa kutosha kichwani, konde ambalo lilimpeleka chini mbabe huyo. Holm hakupoteza muda na kuendelea kumshambulia kwa makonde akiwa chini kabla ya refa kuingilia kati na kumuokoa.

Ronda Rousey

Kichapo hicho cha ‘Knock Out’ kilivuruga rekodi ya Rousey na kukomesha utemi wake wa kutopigwa katika mapambano makubwa 12 mfululizo.

Rousey alikuwa na rekodi ya kutisha kwa kushinda mapambano 11 kati ya 12 katika mzunguzo wa kwanza. Ubabe huoulimfanya hadi afikie hatua ya kumtambia mbabe wa ndondi duniani, May Weather.

 

Kibadeni Aanika Kikosi Cha Kilimanjaro Stars
Ali Kiba Anaamini Pesa Imetumika Kumhujumu Tuzo Za AFRIMMA