Kampuni ya KenSalt ya nchini Kenya, imetangaza kuongeza bei ya chumvi kuanzia hii leo Aprili 15, 2023 kwa sababu ambazo hazikuweza kuainishwa mara moja nchini humo na kuzua manung’uniko miongoni mwa Wakenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Arpan Roy, imeujulisha umma kuwa wanunuzi wa chumvi watalazimika kulipa shilingi elfu moja zaidi kwa kila tani ya chumvi pamoja na ushuru.

Amesema, ongezeko hilo ni la shilingi moja zaidi kwa kila pakti ya kilo moja ya chumvi na hivyo wanunuzi wanatakiwa kuzingatia mabadiliko hayo huku wengi wakilalamikia upandaji wa bei za bidha muhimu kwa jinsi unavyoshika kasi maeneo mengi.

Hivi karibuni, Kinara wa muungano wa Azimio Raila Odinga alisema kuwa mandamano yao ya kitaifa yataendelea licha ya mazungumzo kuandaliwa, amesema atatangaza siku mpya za maandamano baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kutamatika kupinga hali ngumu inayowakumba Wakenya.

Waziri Mkuu arushiwa bomu akihutubia, mshukiwa akamatwa
Juma Mgunda: Tupo tayari kupambana