Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco imethibitisha rasmi kumkamilisha usajili wa kiungo Clatous Chama kutoka klabu ya Simba SC kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kiungo huyo wa Kimataifa wa Zambia, alisajiliwa na Simba mwaka 2018 akitokea katika klabu ya Lusaka Dynamos ya nchini humo.

Ameichezea Simba kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kusaidia timu hiyo kufika hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Chama anaenda kuungana na Tuisila Kisinda, raia wa Congo aliyewahi kukipiga katika Klabu ya Yanga SC na sasa yupo Berkane ambako ameenda kuendeleza maisha yake ya Soka baada ya kuuzwa na klabu yake hiyo ya zamani.

Mwanafunzi ajinyonga baada ya kusimamishwa masomo
Usajili DTB FC balaa tupu