Kitengo cha utatibu cha klabu ya Real Madrid, kimemthibitishia meneja wa klabu hiyo Zinedine Zidane, kuwa anaweza kumtumia mshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo katika mchezo wa hii leo, ambao utaamua hatma yao ya kutinga kwenye hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Man City.

Taarifa zilizothibitisha na kitengo hicho kwenda kwa Zidane zinaeleza kwamba, Ronaldo yupo fit kwa asilimia mia moja (100%) hivyo ni jukumu lake kumtumia katika mpambano wa hii leo ama kumuweka benchi.

Zidane alipokutana na waandishi wa habari kuelekea katika mchezo wa hii leo alisema Ronaldo yupo vyema na amefurahishwa na hatua hiyo, hivyo hana shaka na mpambano ambao utakwenda kuamua nani atajiunga na Atletico Madrid katika safari ya mjini Milan nchini Italia ambapo ndipo fainali ya mwaka huu itakapochezwa.

“Cristiano yupo vizuri tena kwa asimilia  100 na ninakuhakikishieni atacheza mchezo dhidi ya Man City.” Alisema Zidane

Katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa juma lililopita nchini England, Ronaldo alikua jukwaani akishuhudia mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Chelsea, Arsenal, PSG Zatunishiana Misuli Kwa N’golo Kante
Ramadhan Chombo Redondo Awatahadharisha Young Africans