Kiungo wa Mbeya City FC,  Ramadhani Chombo ‘Rendondo’ ameionya  timu ya Yanga  ya jijini Dar Es Salaam  kuwa  ijiandae vya  kutosha itakapokuja  jijini hapa mwanzoni mwa juma lijalo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania  bara uliopangwa  kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mei 10 mwaka huu.

Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo, Redondo  aliyekosa michezo miwili ya awali kupisha majeraha ya mguu kabla ya kurejea na kuichezea City kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar aliweka wazi kuwa ana imani kubwa na kikosi cha sasa cha timu yake, hasa baada ya ujio  kocha Kinnah Phiri aliyefanikiwa kuyaondosha ‘makandokando’ yote yaliyokuwa nasababisha timu kufanya vibaya kwenye michezo iliyopita.

Nadhani Yanga wanatakiwa wajiandae vizuri, wanakuja  kukutana na kikosi  cha City ambacho kiko kwenye  wakati mzuri  hivi sasa,hivyo wasitegemee mteremko,ujio wa kocha  Phiri  umeiimarisha zaidi timu yetu, ametupa muongozo mzuri na amefanya kazi kubwa  kuweka timu sawa, hivyo hao wanaokuja wajue watakutana na upinzani mkali,timu yetu  sasa inacheza tofauti sana na ilivyokuwa inacheza hapo mwanzo, alisema.

Akiendelea  zaidi Redondo, aliyewahi kucheza kwa mafaniko kwenye  timu za Ashanti, Simba na Azam Fc alisema kuwa  anafahamu mchezo huu utakuwa mgumu pande zote  kwa sababu kila timu inahitaji matokeo kulingana na  hali ilivyo kwenye msimamo, Yanga  ikitaka  kujihakikishia ubingwa na City ikihitaji kujiweaka kwenye mazingira mazuri zaidi licha ya kuwepo kwa uhakika kuwa itasalia kwenye ligi .

Kuhusu majaaliwa yake kwenye kikosi cha City Redondo alisema kuwa  anaimani kubwa  atakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao, na kuweka wazi furaha yake  ya  kuwa mchezaji wa timu hii tangu alipojounga nayo mapema  mwezi Januari.

“Nilijiunga na City mapema mwezi januari, nakumbuka  ilikuwa ni wakati wa usajiri wa dirisha dogo,  binafsi nina furaha  hapa na nitaka kufanya  kazi zaidi  na kwa uwezo wangu wote kwa sababu  lengo langu ni kuendelea kuwepo, kwa ngumi mimi  hii ni timu nzuri  kuliko zote nilizowahi kucheza, kuna wakati najiuliza kwa nini sikuwa huku mapema  lakini  hii ni soka na maisha ya mchezo huu ndiyo yalivyo”  alimaliza

Tangu alipojumuishwa  kwenye kikosi cha  City, Ramadhani Chombo ‘Redondo’, amecheza mechi 8 na kufunga mabao  2, huku pia akiwa na rekodi ya kadi 2 za njano hadi sasa.

Cristiano Ronaldo yupo Fit Kwa Asilimia 100
Azam FC Vs JKT Ruvu Himid, Wanga Kurejea kikosini, Aggrey, Migi Nje