Uongozi wa klabu ya yanga umeshangazwa na maamuzi ya mchezaji wao Andrew Vincent ‘Dante’ kufungua mashtaka ya kudai fedha zake ambazo ni zaidi ya milioni 45 katika Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF).

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, ambaye alizungumza na moja ya chombo cha habari nchini ameeleza kuwa kwa namna hali yao ilivyo ndani ya klabu yao ni ngumu kumlipa Dante kiasi chote hicho cha pesa.

Bumbuli amesema hapo awali walikubaliana naye kuwa watakuwa wanalipana kidogokidogo lakini baadaye wamekuja kushangazwa na namna alivyoamua kwenda TFF kushtaki.

”Ujue sisi na Dante awali tulikubaliana naye tuwe tunamlipa kidogokigo.

“Kwa kiasi cha pesa aliyonayo na hali iliyopo Yanga ni ngumu kumlipa fedha yake yote.

“Tunashangaa kuona amekimbilia TFF ambao hawawezi hata kumpa fedha hiyo labda wawe wanakata kutokana na mapato ya uwanjani.”

Dante alifikia maamuzi hayo baada ya kuona fedha zake hazilipwi hivyo kuamua kuangalia sehemu nyingine ya kudai haki yake na ndipo aliona TFF panafaa.

Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa EAC kuanza kesho jijini Arusha
Lampard 'akomalia' mapambano kwa vigogo Uingereza