Chama cha soka nchini England (FA) kimemfungilia mashtaka meneja wa klabu ya Sunderland, David Moyes kufuatia utovu wa nidhamu aliouonyesha wakati wa mchezo wa kombe la ligi (EFL Cup) dhidi ya Southampton usiku wa kuamkia jana.

Meneja huyo kutoka nchini Scotland, alimbwatukia mwamuzi Chris Kavanagh kwa madai alikua anakiminya kikosi chake kwa maamuzi ambayo alihisi hayakuwa sahihi.

Sauti ya kufoka ya meneja huyo ilisikika dhahir pale Maya Yoshida alivyomtendea ndivyo sivyo Victor Anichebe katika eneo la hatari, jambo ambalo lilimkera Moyes kwa kuamini Sunderland walinyimwa penati kwa makusudi.

Kufutia kauli ya kufika, mwamuzi Chris Kavanagh alimuamuri  Moyes kuondoka katika eneo lake la kazi na kwenda kukaa jukwaani kwa usaidizi wa mwamuzi namba nne James Adcock.

Mchezo huo ulishuhudia Sunderland wakitupwa nje ya michuano ya EFL Cup kufuatia kufungwa bao moja kwa sifuri.

Georges Leekens Abebeshwa Mikoba Ya Milovan Rajevac
Serikali kuchukua rasmi shamba la Sumaye, 'hatuangalii sura ya mtu'