Wawakilishi pekee wa nchini England katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya katika hatua ya nusu fainali, Man City wapo njia panda kuikosa huduma ya kiungo mchezeshaji kutoka nchinio Hispania, David Silva kuelekea katika mpambano wa mkondo wa pili dhidi ya Real Madrid.

Sintofahamu kwa kiungo huyo imetokea baada ya Silva kuumia katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo ambapo ilishuhudia Man City wakishindwa kuunguruma katika uwanja wao wa nyumbani (Etihad Stadium) na kujikuta wakilazimishwa matokeo ya sare ya bila kufungana.

Silva alilazimika kutoka nje ya uwanja na nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji kutoka nchini Nigeria Kelechi Iheanacho, kipindi cha kwanza katika mchezo huo baada ya kupata majeraha ya misuli hatua ambayo ilitoa msukumo kwa meneja wa Man City Manuel Pellegrini kusema kuwa hana uhakika kama kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 atakuwa amepona kabla ya kati kati ya juma lijalo.

“David alikuwa mzito kidogo, ni ngumu kusema kwa sasa lakini ni ngumu kwake kupona ndani ya wiki moja,” alisema Pellegrini.

Man City watafunga safari ya kuelekea mjini Madrid tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili ambao umepangwa kuchezwa siku ya jumatano juma lijalo, na itawalazimu kusaka ushindi ama matokeo ya sare ya mabao ili wajihakikishie kutinga katika mpambano wa hatua ya fainali ambao utachezwa mjini Milan nchini Italia Mei 28.

Kolo Toure Achimba Mkwara Mzito Liverpool
Chicharito Afichua Siri Ya Kujiunga Na Bayer 04 Leverkusen