Mshambuliaji kutoka nchini Mexico na klabu ya Bayer 04 Leverkussen ya nchini Ujerumani, Javier Hernández Balcázar “Chicharito” amefichua siri ya kukubali kucheza katika ligi ya Bundesliga.

Chicharito amesema wakati akiondoka Man Utd mwanzoni mwa msimu huu, klabu kadhaa na zenye majina makubwa barani Ulaya zilionyesha nia ya kutaka kumsajili, lakini alizipiga chini.

Akizungumza na Gazzetta dello Sport, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alisema klabu za nchini Italia zilionyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili lakini alichagua kujiunga na Leverkusen kwa sababu aliona wana nafasi nzuri ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Juventus, Inter Milan, AC Milan, SS Lazio na AS Roma walijaribu kunisajili katika kipindi cha joto,” alisema Chicharito.

“Nilichagua Leverkusen sababu ya Ligi ya Mabiingwa Ulaya na walinifanya nihisi nahitajika. Walinishawishi na ninatakiwa niwasaidie na hilo litanifanya nitabasamu kila wakati … nina mkataba nao mpaka 2018 na nina kila kitu ninachohitaji pale” aliongeza Chicharito

David Silva Amuweka Njia Panda Manuel Pellegrini
Tiboroha: Sina Mpango Wa Kugombea Nafasi Yoyote