Mkali wa Skeluwu, Davido ambaye awali alikuwa na mgogoro na Diamond Platnumz kabla hajatangaza kuuweka kando, ameongeza orodha ya wasanii wakubwa waliompongeza baada ya kushinda MTV EMA.

Kupitia Instagram, Davido ameungana na Swiz Beatz, Ne-Yo na wasanii wengine wakubwa duniani na Afrika kumpongeza Diamond kwa kushinda tuzo ya Worldwide Act, Africa/India MTV EMA, tuzo kubwa ambayo haijawahi kushikwa na msanii yoyote wa Afrika.

DIAMOND 1

“CONGRATS BROTHER!!! @diamondplatnumz I remember when I first met u!! GOD HAS BLESSED U …. PROUD OF YOU.” Amendika.

Diamond alikuwa akishindania tuzo hiyo na mshindi wa Miss World 200 ambaye pia ni muigizaji na mwanamuziki, Priyanka Chopra.

Kinachoendelea Mwanza Kati ya Mabula na Wenje
Maalim Seif Ajitoa, Aweka Takwimu Zake Hadharani