Sintofahamu imeendelea katika jimbo la Nyamagana jijini Mwanza ambapo mvutano mkali umeripotiwa kati ya Stanslaus Mabula wa CCM na Ezekiel Wenje wa Chadema na kusababisha matokeo kucheleweshwa.

Ripoti kutoka jijini humo zimeeleza kuwa kumetokea mkanganyiko wa mahesabu ya kura ambayo yamepelekea mvutano mkubwa kati ya pande zote mbili ambapo imedaiwa kuwa wagombea hao wameshindwa kuelewana kuhusu matokeo yaliyojumuishwa kutoka katika vituo mbalimbali vya kupigia kura.

Wenje ambaye alikuwa ni mbunge anaetetea nafasi hiyo alitaka kura hizo zihesabiwe upya na zikarudiwa mara nne bila makubalino tangu majira ya saa mbili asubuhi. Kwa mujibu wa ripota wetu kutoka Mwanza, imeamliwa kuwa kura hizo zihesabiwe kwa mara ya mwisho na mshindi kutangazwa bila kurudia tena.

Katika hatua nyingine, Katika jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Angelina Mabula wa CCM ameshinda kwa kura 85,424 dhidi ya Hainess Kiwia wa Chadema aliyekuwa mbunge, ambaye amepata kura 21, 676.

Halima Mdee Afunguka Baada Ya Taarifa Kusambaa Kuwa Ameshindwa Mapema
Davido, Swizz Beatz, Neyo Wampa Shavu Diamond Kiroho Safi