Wakati kukiwa na taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa mbunge wa Kawe kupitia Chadema anaetetea kiti chake katika saa chache zilizobaki, Halima Mdee ameshindwa, amejitokeza na kukanusha taarifa hizo.

Mdee ametumia akaunti yake ya Twitter kumjibu mtu aliyekuwa na shauku ya kufahamu kilichomsibu kisiasa na kwanini amekuwa kimya muda mrefu, ambapo alimjibu kuwa yuko busy na matokeo huku akijigamba kuwa amempita kwa mbali mshindani wake wa CCM, Kippi Warioba.

“Niko busy na matokeo… Nimemkimbiza KIPPI vibaya. Now niko Osterbay chumba cha majumuisho. Na yeye anajua!” alitweet.

Kada huyo wa Chadema hakusita kumjibu kwa tambo mtu mmoja aliyempa pole kwa madai kuwa amepata ajali ya kisiasa.

“Kama mlipanga kujitangazia ushindi imekula kwenu. Nina matokeo yote. Kila kituo. Nimekimbiza mbaya,” inasomeka tweet ya Halima Mdee.

Kubenea Alia Na Tume, Wenje Yawemkwisha
Kinachoendelea Mwanza Kati ya Mabula na Wenje