Shirika la maji safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limetangaza kuwa siku ya Juma tatu Julai 31, 2017 mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa saa 8, kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 11:00.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Meneja uhusiano wa DAWASCO, Everlasting Lyaro imeeleza kuwa sababu za kuzimwa mtambo huo nikuweza kumruhusu mkandarasi wa (WABAG) kukamilisha mfumo wa umeme katika mtambo mpya wa uzalishaji maji wa Ruvu juu uliopo mlandizi mkoani Pwani.

Hivyo, DAWASCO imewatangazia wananchi wote wa jiji la Dar es Salaam, Kibaha Mkoani Pwani wanaotumia maji hayo kuwa watakosa huduma hiyo kwa muda wa saa 8 ili kuboresha huduma hiyo.

NEC yatoa ufafanuzi kuhusu uteuzi wa wabunge CUF
Magazeti ya Tanzania leo Julai 30, 2017