Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa amezindua kitabu cha kuzuia na kukabiliana na ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Jitihada zake za kukemea vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii na kuhimiza suala la maadili.
Uzinduzi huo, umefanyika jijini humo chini ya Taasisi inayoziunganisha taasisi za Dini Nchini – TIP, ambapo Mkuu huyo wa Wilaya Malisq alimuwakilisha Mkuu Mkoa wa Mbeya,Juma Homera.
Amesema, TIP inastahili pongezi kwa jitihada za kuandaa kitabu hicho kinachokemea vitendo viovu na kwamba mchango wa wadau wakiwemo UNICEF na UNFPA, umesaidia kuleta hamasa katika kupingana na vitendo vya unyanyasaji katika jamii.
Aidha, Malisa pia amesisitiza wadau kupeleka elimu ya Maadili Shuleni na katika ngazi za familia, ili jamii ipate kunufaika na elimu ya maadili.