Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amekabidhiwa jengo la ofisi ya Walimu lenye thamani ya dola za Marekani 94.5 kutoka Serikali ya watu wa Japan pamoja na madarasa matatu Kwa ajili ya Shule ya Msingi Gogo iliyopo Zingiziwa Wilayani Ilala jijini Dar es salaam.

Makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Salam jana ambapo Balozi wa Japan nchini Tanzania Shinichi Goto alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala.

Akipokea msaada huo wa jengo la Utawala Shule ya Gogo, Mjema aliipongeza Serikali ya Japan kwa ushirikiano wao kusaidia kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli za kutoa elimu ya Msingi bila ya malipo inayokwenda sambamba na kuboresha miundombinu ya elimu nchini.

“Katika shule hii ya Gogo Manispaa ya Ilala tutatoa Wataalamu wa kisasa wa Sayansi, waje waendesha ndege na Wahandisi watatoka katika shule hii kwani ujenzi huo umekuja wakati mzuri katika shule za Serikali ya Manispaa ya Ilala matokeo ya darasa la saba mwaka 2018 Mwanafunzi wa kwanza pia ametoka shule hiyo,” amesema Mjema.

Amesema kuwa Mradi huo unatarajia kuwa na faida kubwa mfano kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani, kupunguza utoro kwa wanafunzi, umeboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza pia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Kwa upande wake Mkurungezi wa Manispaa ya Ilala, Jumanne Shauri amesema kuwa Mradi wa upanuzi wa Shule hiyo ulianza Mei 2018 kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, Halmashauri pamoja na Jamii, utekelezaji wa Mradi huo umehusisha, ujenzi wa jengo la Utawala, vyumba vitatu vya madarasa pamoja na thamani za ofisi na kalo la maji taka.

Naye Balozi wa Japani Nchini Tanzania, Shinichi Goto amesema kuwa mradi huo utasaidia kutoa mazingira mazuri ya kusoma pamoja na kufundishia ambapo Shule hiyo itakuwa mfano Kwa Shule zingine.

 

 

Tanzania ya zamani ilikuwa ikiishi kama nchi yenye Laana- Askofu Kakobe
Treni ya kifahari yaleta Watalii 61