Uongozi wa klabu ya Aston Villa umetangaza kumfukuza kazi Roberto Di Matteo, baada ya kufanyanae kazi kwa siku 123 kama mkuu wa benchi la ufundi.

Di Matteo anaondoka Villa Park huku akiiacha Aston Villa ikishika nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi daraja la kwanza nchini Uingereza (Sky Bet Championship), licha ya kutumia kiasi cha Pauni milioni 50 wakati wa usajili wa majira ya kiangazi.

Di Matteo alitangazwa kuwa meneja wa Aston Villa mwezi Juni mwaka huu, na aliaminiwa huenda angefikia malengo ya kuirejesha klabu hiyo katika mshike mshike wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza (PL) lakini imekua tofauti.

Katika utendaji wake wa kazi tangu mwanzoni mwa msimu huu, meneja huyo kutoka nchini Italia amefanikiwa kushinda mchezo mmoja wa ligi daraja la kwanza kati ya michezo 12 aliyocheza hadi mwishoni mwa juma lililopita.

 

Luis Enrique: Nipo Tayari Kulaumiwa Na Yoyote
Video: Tamko la Waziri Mkuu kuhusu wadaiwa sugu taasisi za Serikali