Nyota ya Diamond Platinumz ni kali na imebarikiwa kwelikweli hadi kuwavuta hata wale ambao alikuwa anatamani japo apige nao picha.

Mkali huyo wa ‘ngololo’ kutoka Tandale, amesema kuwa viatu vyake pekee ndivyo vilikuwa ulimbo wa kumvuta kwake rapa Kanye West, aliyetamani kukipiga picha bila kutambua kuwa Diamond yeye alitamani kupiga naye picha.

“Nilipokuwa airport pale Los Angeles tunasubiri kuchukua mabegi yetu, nilisikia mtu akisema ninaweza kupiga picha viatu vyako? Kwakuwa alikuwa ameinama sikuweza kumtambua lakini alipoinuka nikashangaa kumuona ni brother Kanye West. Nilimuomba tupige picha kwanza halafu vingine vitaendelea,” Diamond ameeleza.

Diamond hakuipoteza hata sekunde moja aliyoongea na Kanye West, msanii alimuweka kwenye level za kimataifa ‘D’ Banj’ baada ya kuonana nae siku moja tu.

“Tumuombe Mungu mambo yaendelee vizuri kama tulivyopanga. Kuna kitu kizuri kinaweza kutokea kati yetu,” alisema Diamond.

Bomu lililolipua nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar lazua haya
Mkwasa Ampa Ushauri Wa Bure Nadir Haroub ‘Cannavaro’