Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema hawezi kuingilia uamuzi wa beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuamua kustaafu kuichezea Taifa Stars.

Mkwasa amesema anaamini Cannavaro anahitajika, hivyo ni vizuri akubali kuendelea kulitumikia taifa lake.

“Mabeki wako wengi sana lakini Cannavaro bado anahitajika,” alisema.

“Lakini namshauri atumie busara na kuliangalia suala hili. Arejee na kulitumikia taifa lake.”

Cannavaro aliamua kuachana na Taifa Stars baada ya Mkwasa kutangaza kumvua unahodha wakati akiuguza majeraha yake baada ya kuumia wakati akiitumikia Stars dhidi ya Algeria.

Uamuzi ambao ulionekana kupingwa na wadau wengi wa soka ambao waliamini Mkwasa hakuutoa wakati sahihi.

Diamond aeleza kitu kilichomvuta Kanye West kwake na Mpango kati yao
Viungo Wa Young Africans Na Azam FC Watajwa Amavubi