Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameandika historia nyingine tena baada ya kutia saini mkataba na kampuni ya muziki ya Afrika Kusini, Warner Music.

Mkataba huo mpya utahakikisha kuwa WCB Wasafi imejumuishwa katika Warner Music Afrika Kusini na Ziiki Media, wakati mtandao wa Warner Music ukisaidia kumfanya Diamond Platnumz na wasanii wa lebo hiyo kupanda hadhira ya ulimwengu.

Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii waliofaulu zaidi Afrika, akiwa ameachia nyimbo zaidi ya 30, ukurasa wake wa YouTube ukiwa na zaidi ya mashabiki milioni tano waliojisajili, na pia ana zaidi ya wafuasi wa Instagram milioni 12.

Mashambulizi Gaza: Zaidi ya Wapalestina 200 wauawa
Kimbunga Tauktae chasababisha vifo