Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, kuanza mipango ya kuongeza Bajeti ya Maji kwa wilaya ya Momba baada ya kufanya ziara na kufanya tathmini ya uhitaji wa jimbo hilo.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya Diwani wa Kata ya Kamsamba Wilayani Momba, Kyalambwene Joshua Kakwale kujilaza chini kama ishara ya msisitizo kumuomba Waziri wa Maji Jumaa Aweso afanikishe Kata hiyo kupata maji kwani Wakazi wake wanateseka ikiwemo baadhi ya Watu kuliwa na mamba wakati wakitafuta maji mtoni.

Akijibu ombi la Diwani, Aweso ameahidi kupeleka kiasi cha shilingi 500 milioni ndani ya wiki mbili kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji utakao kuwa suluhu ya changamoto ya Maji katika eneo hilo lenye wakazi wengi, huku akiwaahidi ndani ya miezi mitatu mradi utakamilika na huduma kupatikana.

Ukuaji wa Teknolojia utaziathiri AZAKI - Dkt. Ndugulile
Ufahamu ugonjwa wa Tetenasi: Chanzo, dalili na tiba