Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemchagua mheshimiwa Dk Tulia Akson Mwansasu kuwa Naibu Spika.

Dk Mwansasu amechaguliwa kwa kura 250 kati ya 351 zilizopigwa ambazo ni sawa na asilimia 71.2.

Mheshimiwa Magdalena Sakaya aliyekuwa akiwania pia nafasi hiyo amepata kura 101 ambazo ni sawa na asilimia 28.8.

Tayari Naibu Spika huyo ameapishwa tayari kwa kuanza kulitumikia bunge hilo.

Kocha Wa Soka Aukwaa Uwaziri Mkuu
Bunge lampitisha Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu