Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godwin Ole Mollel ambaye alihama chama hicho na kujiunga na CCM amesema kuwa alipotoka Bungeni wakati Rais Dkt. Magufuli anaingia ulikuwa ni uamuzi wa kitoto.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 ambapo Mollel sasa anagombea ubunge wa jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Nilipofika Bungeni nikaambiwa ukimuona Magufuli anaingia Bungeni wewe toka nje, nikabisha kidogo nikaambiwa wewe ambaye ni mbishi kwanza tangulia mbele, kwa sababu mimi nina nidhamu na naheshimu viongozi nikatangulia kikamanda mbele nikatoka nje, nikiumia nikisema nimefanya jambo la kitoto lakini ikafika mahali nikaambiwa hauruhusiwi kuongea na Mbunge wa CCM, wala kumsalimia”amesema Mollel

Amesema kuwa baadaye aliambiwa ashone suti ili siku bajeti ikiwa inajadiliwa watoke nje lakini yeye anadai aligoma na kuanzia hapo alianza kuchukiwa ndani ya chama chake hicho alichokihama.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Lowassa ataenda kupiga kampeni za CHADEMA Siha na kusema anatambua kiongozi huyo amepangwa na hawezi kukataa kwa kuwa anaogopa kufukuzwa kwenye chama kwa kuwa tayari yeye ni mzee lakini amesema alishawaeleza ukweli kutoka Ikulu kwamba CCM ndiyo mpango.

Nyosso amshushia makonde shabiki wa Simba
Magazeti ya Tanzania leo Januari 23, 2018