Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Bodi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi wa TRC kuendelea kutimiza wajibu wao wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati ili iweze kukamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.

Dkt. Mpango, ameyasema hayo wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa wa Reli ya Kisasa (SGR), Kipande cha nne Tabora – Isaka wenye urefu wa Kilometa 165 inayogharimu shilingi Trilioni 2.09 iliofanyika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame
Mbarawa pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali akiweka Majina ya Viongozi na Wataalamu mbalimbali waliohusika katika mchakato wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka.

Amesema, Viongozi hao wanatakiwa kuongeza uzalendo, kujituma, kuwa wabunifu, kufanya kazi kibiashara kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo, huku akiwataka mkandarasi wa reli ya kisasa kipande cha nne Tabora – Isaka kuhakikisha vijana wa mkoani Shinyanga na Tabora wanapewa kipaumbele katika fursa mbalimbali za ajira zinazoweza kutolewa kwa kundi hilo.

Aidha, Dkt, Mpango pia ametaka kuwapo kwa fursa kwa wakinamama upande wa utoaji wa huduma mbalimbali kama za chakula, ili mradi huo uweze kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo na mikoa jirani na kwamba vyombo vya ulinzi na usalama viwashughulikie wanaohujumu ujenzi wa mradi huo.

Waziri Kairuki akemea Viongozi waomba rushwa
Makamu wa Rais akemea wizi, uchepushaji wa maji