Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema Serikali itaendelea kugharamia utekelezaji wa miradi ya kimkakati, ili kuhakikisha inakamilika na kuchangia katika ukuaji wa
uchumi wa wa taifa.

Dkt. Mpango, ameyasema hayo wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa wa Reli ya Kisasa (SGR), Kipande cha nne Tabora – Isaka wenye urefu wa Kilometa 165 inayogharimu shilingi Trilioni 2.09 iliofanyika eneo la Isaka, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame
Mbarawa pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali akiweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka yenye urefu wa Kilometa 165 katika hafla iliofanyika Isaka Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka yenye urefu wa Kilometa 165 wakati wa hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli hiyo iliofanyika Isaka Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Shirika la Reli
Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa wakati akitembea katika mfano wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango wakati akihutubia Viongozi,Wakandarasi ,Watumishi wa TRC pamoja na wananchi mbalimbali wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka yenye urefu wa Kilometa 165.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali na
Wakandarasi wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka.
Sehemu ya Wananchi waliohudhuria hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Kipande cha nne Tabora – Isaka.

PAC yawatimua kikaoni wafanyakazi wa Wizara
Polisi yatawanya maandamano ya Wanaharakati