Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amemuagiza Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kusimamia mahusiano ya kifedha baina ya pande mbili za Muungano wa Tanzania.

Dkt. Mpango ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango kabla ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania Machi 30 mwaka huu, ametoa agizo hilo jana Aprili Mosi 2021, Ikulu Jijini Dodoma wakati wa uapisho wa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mawaziri na Manaibu Waziri.

Dkt. Mpango amewataka Waziri Mwigulu pamoja na Waziri wa Muungano na Mazingira, Seleman Jafo kuanza wakishirikiana na Manaibuu wao kuanza na utatuzi wa mahusiano ya kifedha baina ya pande zote za Muungano.

Aidha, ametoa onyo kwa Makatibu na Manaibu Makatibu kutokuwa na mivutano na kufanya kazi kwa umoja ambapo amemwambia Katibu Mkuu Balozi Hussein Kattanga kufikisha salamu hizo na kuwaambia kuwa anafuatilia swala hilo hivyo wawe makini katk ushirikiano wao wa utendaji kazi.

Madareva 10 wa mabasi wafungiwa kwa mwendokasi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 2, 2021