Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, amezipongeza Serikali za Cuba na Oman kwa kuendelea kuunga mkono  Zanzibar katika kuendeleza miradi ya maendeleo sambamba na kuimarisha uhusiano wa ushirikiano wa kihistoria kati ya nchi hizo.

Ameyasema hayo wakati alipokutana na mabalozi wa nchi hizo Ikulu Mjini Unguja, Dkt. Shein amezipongeza nchi hizo  kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria  ambao umekuwa chachu ya kuimarisha uhusiano.

Aidha kwa upande wake Balozi wa Cuba anaemaliza muda wake hapa nchini Jorge Tormo, amemuhakikishia  Dkt. Shein kuwa uhusiano utaendelea kuimarika kadri siku ambavyo zinavyoenda.

Kwa upande wake Balozi wa Oman, Ahmed bin Humoud Al Habsi, amesema kuwa nchi yake itaendeleza uhusiano na Zanzibar ili kuweza kuimarisha shughuli za kimaendeleo na kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

 

Machinga wageuka ‘pasua kichwa’ Morogoro
Kampuni za simu nchini hatarini kufungiwa