Tajiri Donald Trump anayewania kuchaguliwa kuwa mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya Republican ameendelea kutoa kauli kushangaza dunia ambapo hivi karibuni amezigeukia nyumba za ibada.

Akiongea katika mahojiano maalum, Tump amesema kuwa atakapokuwa rais wa Marekani atafikiria kwa kiwango kikubwa kufunga baadhi ya Misikiti nchini humo.

Trump ambaye amekuwa akitoa kauli nyingi zinazosadikika kuwa za kibaguzi, alisema kuwa anaamini kauli nyingi za chuki na uchochezi hutoka katika maeneo hayo.

“Hii ni kwa sababu mawazo na chuki yanatoka katika baadhi ya maeneo hayo,” alisema.

Wachimbaji Watano Waokolewa Baada Ya Kuishi ‘Kimiujiza’shimoni Siku 41 Wakila Mende
Majanga Yarejea Tena Muhimbili Baada ya Rais Kuyaondoa