Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji, Eden Hazard anahusishwa na taarifa za kutikisa kibiriti, ndani ya klabu ya Chelsea kwa kuushinikiza uongozi kukubali kumuachia na kujiunga na Real Madrid.

Taarifa za kuwepo kwa kutikisa kibiriti kwa mchezaji huyo, zimeibuliwa na gazeti la L’Equipe la nchini Ufaransa ikiwa ni siku moja baada ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ublegiji Mack Wilmot, kushauri Hazard kuondoka Chelsea ili kupata nafasi ya kuonyesha kiwango chake ipasavyo.

Taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la L’Equipe, zinadai kwamba Hazard amekua hana furaha ndani ya klabu ya Chelsea kama ilivyokua miaka ya nyuma wakati aliposajiliwa akitokea Lille ya nchini Ufaransa.

Hali hiyo inatajwa kuwa chanzo cha mchezaji huyo kuonyesha kiwango duni tangu msimu huu ulipoanza, ikilinganishwa na msimu uliopita ambapo alichangia kwa kiasi kikubwa Chelsea kutwaa ubingwa wa nchini England.

Hata hivyo, suala la kuhitaji kuhama liliibuliwa mapema na Hazard mwenyewe, baada ya kuandika kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram amekua akitakiwa kwa udi na uvumba kwenye klabu ya Real Madrid.

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, aliamuacha nje ya kikosi cha kwanza, Hazard wakati wa mchezo wa ligi ya nchini England wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Aston Villa ambao walikubali kuchapwa mabao mawili kwa sifuri.

Hazard, alirejeshwa kikosini katika mchezo wa usiku wa kuamkia jana wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, ambapo Chelsea walipambana na Dinamo Kiev na kuambulia matokeo ya sare ya bila kufungana.

Magufuli: Hakuna Anaenidai…
Louis van Gaal: Anthony Martial Ni Mpumbavu