Chama cha soka nchini Misri (EFA) kimetangaza nafasi 50,000 kwa mashabiki ambao wataruhusiwa kushuhudia mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia kati ya timu ya taifa hilo dhidi ya Ghana, ambao umepangwa kuunguruma Novemba 13 mjini Alexandria.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa katika uwanja wa Borg El Arab na utakua chini ya uangalizi mkali wa kiusalama, kwa ajili ya kuhofia fujo ambazo mara kadhaa zimekua zikianzishwa na mashabiki wan chi hiyo.

Katika hatua nyingine EFA wametoa nafasi kwa mashabiki 40,000, kuhuhudhuria uwanjani hapo kwa ajili ya kushuhudia mpambano wa mkondo wa pili wa hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika, kati ya  Zamalek dhidi ya Mamelodi Sundowns utakaochezwa Oktoba 23.

Mchezo wa mkondo wa kwanza kati ya wawili hao ambao ulichezwa Afrika kusini mwishoni mwa juma lililopita ulishuhudia wenyeji Mamelodi Sundowns wakichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.

Kitendawili Cha Makundi Ya Afrika Kuteguliwa Mjini Libreville
Vumbi La Ligi Ya Mabingwa Ulaya Lazidi Kutimka