Mshambuliaji wa Tanzania, Elias Maguli amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini.

Kabla ya kujiunga na Polokwane, Maguri alikuwa akiichezea timu ya Dhofar FC ya Oman tangu Juni 2016 akitokea Stand United ya Tanzania.

Kukamilika kwa dili hilo la kujiunga na Polokwane kunamaliza tetesi za striker huyo kujiunga na vilabu vya Simba na Yanga ambavyo awali vilihusishwa kuwania saini yake katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili nchini.

Kutokana na usajili huo, sasa Maguri anaungana na Abdi Banda anayeichezea Baroka FC ya Afrika Kusini huku wote kwa pamoja wakiwa ni wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Kwa sasa Maguli yupo na timu ya taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ inayoshiriki katika michuano ya Kombe la Chalenji nchini Kenya.

Polokwane baada ya kucheza mechi 11 kwenye Ligi ya Afrika Kusini imefanikiwa kuvuna pointi 11 ikiwa imeshinda michezo miwili, sare tano na imeshapoteza mechi nne, inashika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hiyo.

Mzamiru Yassin azua utata
Ofisi ya msajili yafafanua umiliki wa hisa Simba SC