Wazazi na Walezi wamehaswa kuwalea kimaadili na kuwapa elimu ya dini watoto wao hali itakayowasaidia kuepukana na mienendo na vitendo vya kujihusisha kwenye mapenzi ya jinsia moja ambayo ni kinyume na maadili na tamaduni za Tanzania.
Hayo yameelezwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kharuna Kichwabuta kwenye mashindano ya kuhifadhi Quran tukufu yaliyofanyika uwanja wa Kaitaba yaliyohusisha wanafunzi wa shule za kiislam kutoka mikoa ya Kagera, Arusha na Mwanza.
Shekh Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kharuna Kichwabuta akiongea na hashara iliyohudhuria mashindano ya kusoma Qur’an uwanja wa Kaitaba.
Amesema “hata Ng’ombe, Mbuzi hawajafanya hivyo lakini mwanadamu ambaye anasoma anapata degree anakuja kupandilia dume kwa dume alafu watu wanasema ni ndoa, hiyo sio ndoa. Lakini yote ni kwasababu ya watu kukosa maadili ya dini.”
Baadhi ya washiriki mashindano ya usomaji Qur’an (Wavulana)
Kwa upande wake mshindi wa kusoma Qur’an kwa waliohifadhi Juzuu 30 Jawadu Mzamir amewasisitiza vijana wenzake kujitahidi kusoma dini kwa manufaa yao katika kukuza maadili huku akisema, “nawasihi Vijana wenzangu kuisoma na kuijua dini hii itatusaidia kulinda maadili Yetu na kutojiingiza katika matendo yasiyompendeza Mungu.”
Baadhi ya washiriki mashindano ya usomaji Qur’an (Wasichana)
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi ya waandaaji wa mashindano hayo, Mwl. Karokola Swaibu amesema lengo lao ni kutoa elimu zote (Dini na Mazingira), kwa kuandaa Vijana bora watakaotumikia taifa kwa kumtii MUNGU wao.