Ndoto za kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain za kucheza fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016, zimeyeyuka rasmi kufuatia taarifa iliyotolewa muda mfupi uliopita huko kaskazini mwa jijini London.

Chamberlain, ambaye alitarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya England ambacho kitashiriki fainali hizo zitakazocheza nchini Ufaransa mwezi ujao, atakua nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili kutokana na maumivu yanayomkabili.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22, alikua amepona majeraha yake ya goti na alipokua katika mchezo wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 21 mwanzoni mwa juma hili alijitonesha.

Wenger amesema majibu ya vipimo alivyofanyiwa Chamberlain, yameonyesha anahitaji matibabu maalum na atakapokua anajiuguza itamchukua muda wa miezi miwili kurejea tena uwanjani.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson anatarajia kutangaza kikosi chake May 13 na atawasilisha orodha ya mwisho ya kikosi hicho huko UEFA Juni 2 tayari kwa fainali za matafaifa ya barani Ulaya.

Azam FC Yaanza Safari ya Kuelekea Mkoani Shinyanga
Thibaut Courtois Ashinikiza Bosi Wake Afukuzwe Stamford Bridge