Mlinda mlango wa klabu ya Chelsea, Thibaut Courtois huenda akaondoka Stamford Bridge, endapo uongozi wa klabu hiyo utashindwa kutimiza ombi lake la kutokua tayari kufanya kazi na kocha wa makipa Christophe Lollichon.

Courtois amesema hana furaha ya kufanya kazi klabuni hapo, chini ya utawala wa kocha Christophe Lollichon ambaye amekua akifanya kazi na mlinda mlango Petr Cech aliyeondoka mwanzoni mwa msimu huu na baada ya kujiunga na Arsenal.

Courtois amewasilisha ombi hilo, kwa kuushinikiza uongozi wa klabu ya Chelsea kumpa uhuru meneja mpya Antonio Conte, kuja na kocha wa makipa ambaye anaamini ataweza kufanya nae kazi kwa uhuru zaidi.

Hata hivyo bado haijafahamika kama uongozi wa The Blues utayaafikia maombui ya mlinda mlango huyo kutoka nchini Ubelgiji, kutokana na uaminifu mkubwa waliojiwekea kwa kocha Lollichon, mwenye umri wa miaka 53.

Christophe LollichonKocha wa makipa wa klabu ya Chelsea Christophe Lollichon

Taarifa za awali zinadai kwamba Antonio Conte ataelekea Stamford Bridge na jopo la wasaidizi wake ambapo ndugu yake Gianluca Conte atakua mshauri wa ufundi, Angelo Alessio na Massimo Carrera watakuwa makocha wasaidizi, Mauro Sandreani atakua msaka vipaji pamoja na Paolo Bertelli atakua kocha wa mazoezi ya viungo.

Safu hiyo inadhihirisha Christophe Lollichon ambaye ni raia kutoka nchini Ufaransa, bado ana nafasi ya kuendelea na kazi yake ya kuwa kocha wa makipa klabuni hapo ambayo ameifanya kwa kipindi cha miaka kumi.

England Kumkosa Alex Oxlade-Chamberlain EURO 2016
Aitor Karanka Atibua Mazingira ya Kazi Yake Riverside Stadium