DJ D-Ommy wa Clouds Fm ambaye ni mshindi wa tuzo mbili kubwa za AFRIMMA na Africa Entertainment Awards (AEA-USA) kama DJ Bora Afrika, ameeleza jinsi ambavyo AY na Diamond walivyompa nguvu ya kupanda jukwaa la kimataifa.

Mchezea santuli huyo aliyeanza safari ya u-DJ akiwa na umri wa miaka 12, ameiambia Dar24 katika mahojiano maalum kuwa AY ndiye aliyemfungua macho akimkosoa vikali kwa kutofanya kazi itakayomtoa kimataifa.

“Ay ndio mtu wa kwanza kabisa kuniambia kuhusu suala la mixing. AY alikuwa ananichana sana, ‘ebana nyie ma-DJ wa Bongo wavivu, hamfanyi mixes yaani mko-mko mtu’, yaani hayo maneno yalikuwa yananiumiza sana,” DJ D-Ommy aliiambia Dar24.

D-Ommy ambaye amekuwa akitoa mix kali na kuziweka mtandaoni, alisema kuwa alipata msukumo wa kufanya hivyo pia kutoka kwa AY, siku moja alipompelekea mix ya video ili amsaidie kuipeleka Channel O.

“Alikuwa ananiambia ‘hizi mix unazofanya ziweke online watu wazione’. Kwahiyo kwangu AY ni mtu aliyekuwa ananipush (ananisukuma), ’ebana fanya hivi.. nenda hivi’,” alisema.

AY pia ndiye alimfungulia mlango wa kufanya ziara ya kuzitambulisha mix zake Afrika Mashariki akianza na nchi ya Kenya ambapo alipata connection ya ma-DJ wakubwa kama Joe Mfalme.

Akizungumzia mchango wa Diamond ambaye wamekuwa wakikutana katika matamasha makubwa nchini Marekani na sehemu nyingine, katika kumbi kubwa na kufanya show ya pamoja, alisema kuwa wamekuwa na maono yanayofanana na wote hawaangalii soko la Tanzania au Afrika pekee.

“Diamond Platinumz, mimi na yeye tuna chemistry nzuri na tuna vision moja. Hatu-focus sana labda Tanzania, East Africa au Afrika… yaani tunataka kwenda mbele. Lakini pia tukikutana tunafanya kazi nzuri. Yaani kabla hajaperform, mimi naperform naiandaa crowd yeye akija anaua,” alisema na kuongeza kuwa huwa wanakuwa na chemistry nzuri wakiwa jukwaa moja.

“Pia, Diamond tunaheshimiana, ananipa mawazo sana.  Ni mmoja kati ya vijana ambao ni watu poa sana. Ana ‘fight’ sana, anaona mbali na sio mchoyo wa kutoa ushauri na sehemu anayoweza kusaidia Naseeb sio mchoyo,” alisema.

Angalia hapa video nzima ya mahojiano alivyofunguka mengi kuhusu alichozungumza na Swizz Beatz, siri ya ushindi wake kwenye tuzo, Surprise yake nzito kwenye Fiesta na mengine:

Magufuli amteua Jenerali Mstaafu Waitara kushika bodi ya Tanapa
Maalim Seif ‘ajifunga plasta mdomoni’ akiwa msikitini