Sehemu ya siri ya mwanamke ni kiungo hatari sana ambacho kinahitaji kupewa uangalizi maalum.

Ni sehemu inayohitajika kusafishwa kwa umakini kwa sababu magonjwa husambaa kwa haraka na kwa njia rahisi.

Wazazi na mababu zetu walikuwa wakisema vitu kama ndimu zinastahili kutumiwa kusafisha uke, ili kuepusha harufu mbaya na magonjwa.

Hata hivyo kwa mujibu wa Daktari bingwa wa wanawake katika hospitali ya kimataifa ya Marie Stopes ya mjini Abuja nchini Nigeria anasema kutokana na sayansi, vipo viungo maalum ambavyo vimebuniwa ili kutumiwa kusafisha uke na mfumo wa uzazi na havina madhara.

Dkt. Fatima anasema kuwa kisayansi kila kiungo katika mwili wa binadamu kina kemikali kama vile tindi kali na alkalini kwa kiwango kinachohitajika mwilini ambapo kuwa na wingi wa kemikali hiyo kunaweza kuleta madhara japo kidogo.

“Maji ya limau yanasadikiwa kuwa na kiwango cha juu cha tindikali ambacho ni cha pili kwa ukubwa wakati uke wa mwanamke una kiwango cha kama robo tatu tu ya tindikali, ” anasema Dkt. Fatima.

Wataalamu wa afya wanasema ni hatari kwa mwanamke kutumia limao kujichua kwa wababu maji ya limao yana ukakasi wa hali ya juu, ambao unabadilisha mfumo wa asili wa uke.

Pia, matumizi ya ndimu kusafisha uke kupita kiasi yanaweza kusababisha kusambaa kwa magonjwa katika eneo hilo.

Utumiaji wa limao kusafisha uke pia unaweza kuathiri shingo ya uzazi hali ambayo inaweza kusababisha saratani ya shingo ya uzazi.

Majeraha yatokanayo na kuchubuka kwa sehemu za siri yanayotokana na matumizi ya limao wakati wa kujisafisha yanaweza kuchangia kusambaza virusi vya UKIMWI.

Wanasayansi wamegundua kuwa sehemu za siri ni mahali wanawake wanapenda kusafisha mara kwa mara na japo ni vyema kufanya hivyo wanashauri uangalifu uzingatiwe wakati wa kufanya hivyo ili kujiepusha na maradhi.

Wakati wa kusafisha sehemu za siri wanawake wanashauriwa kutumia maji ya vugu vugu kwa uangalifu kwa sababu yakiwa ya moto zaidi, pia maji hayo yanaweza kusababisha magonjwa mengine.

Bofya hapa chini kafahamu matumizi sahihi na yasiyo sahihi ya limao

Waziri aagiza watumishi wa TBA kukamatwa
Aliyeongoza kidato cha nne aelezea matamanio yake