Klabu ya Barcelona inajiandaa, kuwasilisha malalamiko kwenye mahakama ya kimichezo CAS, huko nchini Uswiz kwa ajili ya kuhitaji ufafanuzi ambao huenda ukawasaidia katika tatizo la usajili kiungo mchezeshaji kutoka nchini Uturuki, Arda Turan.

FC Barcelona wanaamini walipaswa kupewa ruhusa ya kumtumia kiungo huyo kutoka Atletico Madrid wakati wa majira ya kiangazi, lakini adhabu iliyotangwa na FIFA dhidi yao ya kutofanya usajili inawazuia kufanya hivyo.

Barca wameshawashiwa taa ya kijani kumtumia mchezaji huyo itakapofika mwezi januari, ambapo adhabu yao iutakua imemalizika, lakini maafisa wa klabu hiyo ya Cataluña, hawakubaliani na jambo hilo.

Tayari taarifa za utetezi wa kesi watakayoifungua huko CAS zimeshakusanya tangu jana, na wanaamini wana kila sababu ya kupewa haki yao ya kumtumia Arda Turan katika kipindi hiki ambacho wanamuhitaji.

Barceloan waliibua mzozo wa kutaka kuruhusiwa kumtumia Arda Turan katika kipindi hiki, baada ya kuumia kwa kiungo wao kutoka nchini Brazil Márcio Rafael Ferreira de Souza Rafinha.

Barcelona, walimsajili Arda Turan wakati wa majira ya kiangazi, lakini walishindwa kumuidhinisha kukitumikia kikosi chao kutokana na adhabu inayowakabili kutoka FIFA.

Barcelona waliadhibiwa na FIFA, baada ya kubainika walifanya usajili wa wachezaji waliokua chini ya umri wa miaka 18 kwa kuvunja kanuni na taratibu zilizowekwa na shirikisho hilo la soka duniani kote.

Mbali na Rafinha kuwa majeruhi kwa sasa, pia Barcelona inakabiliwa na mtihani wa kuwauguza wachezaji wake muhimu katika kipindi hiki kama Lionel Messi pamoja na Andres Iniesta.

Nahodha Wa Yanga Arejesha Salamu Chamazi
Tanzia: Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, Dkt. Makaida Afariki