Miamba ya Soka Nchini Ujerumani Klabu ya Bayern Munich hadi Sasa imekamilisha Usajili wa Wachezaji Watatu ikiwa ni katika harakati za kuendelea kukiongezea ubora Kikosi kwa ajili ya Msimu Ujao wa Mashindano Mbalimbali.

Bayern Wamemsajili Sadio Mane raia wa Senegal Kutoka Liverpool Kwa Ada ya paundi milioni 43 na kusaini Mkataba wa miaka mitatu hadi mwaka 2025.

Mwingine ni Ryan Gravenberch mwenye umri wa miaka 20 Kutoka Ajax Amsterdam ya Nchini Uholanzi ambaye anacheza nafasi ya Kiungo Mchezeshaji akisaini mkataba wa miaka mitano ambao utamweka Allianz Arena hadi mwaka 2027

Mchezaji Mwingine ni Kutoka hapo hapo Ajax Amsterdam anacheza nafasi ya mlinzi wa kulia Noussair Mazraoui mwenye umri wa miaka 24 ambaye amesaini mkataba wa miaka minne utaomweka Allianz Arena hadi Mwaka 2026.

Treni ya abiria yapata ajali Tabora
Young Africans yagoma kumuuza Feisal Salum