Kiungo kutoka Visiwani Zanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’ ametamba kuwa tayari kwa mchezo wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ dhidi ya Uganda.

Fei Toto ambaye aliwashangaza wengi kufuatia kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ili hali kwa muda mrefu amekua nje ya kikosi cha Young Africans kufuatia mzozo unaoendelea dhidi ya Uongozi wa klabu hiyo, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu utayari wake kuelekea mchezo dhidi ya The Cranes ambao utapigwa kesho Ijumaa (Machi 24) nchini Misri.

Fei Toto amesema: “Kuna wachezaji wapya na mwalimu mpya, Uganda tunawaheshimu, ni timu nzuri, ina wachezaji wazuri, ila tutaipambania Taifa”

“Najua siyo jambo rahisi, lakini ni muhimu zaidi kwa timu yetu kushinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu. Katika mechi mbili Watanzania watuombee dua na tutapata matokeo mazuri kwa uwezo wake Mungu,”

Katika mchezo wa kesho Ijumaa (Machi 24) Uganda watakuwa nyumbani katika Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia-Misri, kabla ya timu hizo kucheza mchezo wa Mzunguuko wanne Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam Machi 28.

Mwezi mtukufu: Waislam watakiwa kutafakari umoja, amani
Mazingira wezeshi uwekezaji yafikisha viwanda 1,522 Pwani