Filamu mpya ya James Bond iliyopewa jina la ‘Spectre’ imeingia sokoni kwa kishindo kikubwa katika wiki yake.

‘Spectre’ iliingia sokoni wiki iliyopita na kuingiza $70.4 Milioni kutoka kwenye majumba ya sinema 3929 yaliyoonesha filamu hiyo wikendi iliyopita.

Hesabu hiyo imeifanya ‘Spectre’ kuwa katika nafasi ya pili ya rekodi za filamu za James Bond kwa kuingiza kipato kikubwa katika wiki yake ya kwanza sokoni ikiifuatia filamu ya ‘Skyfall’ ya mwaka 2012 iliyoingiza $88.4 milioni.

“Ni mwanzo mzuri. Kila bara ikiwa ni pamoja na Latin America, Asia na Ulaya, inavunja rekodi ya ‘Skyfall’,” alisema rais wa usambazaji duniani wa kampuni ya Sony, Rory Bruer.

‘Spectre’ imeongoza kwenye chart za Box Office ikifuatiwa na Peanuts iliyoingiza $ 44.2 milioni NA ‘The Martian’ iliyoingiza $ 9.1 milioni.

 

Mkwasa: Stars Ipo Tayari Kuwavaa Algeria Kesho
Azam FC Kuanzisha Mradi Kuinua Soka La Vijana