Mshambuliaji hatari wa Young Africans Mkongomani, Fiston Kalala Mayele ameweka wazi kuwa walifanya kila kinachowezekana ili kushinda ubingwa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika, lakini waliukosa kwa kuwa haikuwa bahati yao.

Young Africans juzi Jumamosi (Juni 03) usiku walishuka kwenye Uwanja wa 5 July 1962 nchini Algeria kuvaana na USM Alger ya nchini humo katika mchezo wa fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo licha ya ushindi wa bao 1-0, Young Africans walipoteza ubingwa huo faida ya bao la ugenini baada ya matokeo ya jumla ya sare ya mabao 2-2.

Licha ya kupoteza ubingwa huo, Mayele alifanikiwa kuibuka mfungaji bora wa mashindano hayo baada ya kumaliza akiwa ameifungia Young Africans mabao saba akifuatiwa na mshambuliaji wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Ranga Piniel Chivaviro mwenye mabao sita.

Mayele ametumia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo aliandika maneno yafuatayo: “Imekuwa kihistoria, tulikuwa na umakini na nia ya kushinda na baada ya yote ni Mungu aliyeamua vinginevyo na hatuna budi kumpa utukufu wa milele.”

NEMC watakiwa kusimamia katazo matumizi mifuko ya plastiki
Simba SC yavamia kwa fujo Khartoum-Sudan