Jarida ‘Forbes’ limetangaza rasmi orodha ya watu mashuhuri wenye utajiri mkubwa zaidi kwa Mwaka 2022, ambapo kwenye orodha hiyo wameonekana kung’ara wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kanye West na Rihanna.

Forbes limeweka wazi kuwa Rihanna ameendelea kuwa bilionea akiwa na utajiri wa $1.7 Bilioni ambazo ni sawa na takribani Shilingi Trilioni 3.9 za Tanzania, akishika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wasanii wa kike wenye pesa nyingi zaidi duniani.

Naye Kanye West ametajwa kumiliki utajiri wa $2 Bilioni, sawa na zaidi ya Trilion 4.6.

Uwepo wa msanii kwenye orodha ya Forbes humpa faida kadhaa za ziada kwenye biashara yake, ikiwa ni pamoja na kuvutia uwekezaji zaidi, kuongeza imani na thamani kwa wadau wa biashara zake.

Kwa Tanzania, huenda Diamond Platnumz akawa msanii anayetengeneza fedha nyingi zaidi kupitia biashara ya muziki. Kutokana na faida nilizozitaja hapo juu, mara kadhaa amekuwa akieleza kuwa hakuna msanii anayemshinda kwa ukwasi nchini, na kwa Afrika ni wachache sana.

Ingawa hajawahi kuweka wazi utajiri wake, Mei 17 mwaka jana aliikosoa vikali orodha iliyowahi kuwa gumzo mitandaoni iliyomtaja katika nafasi ya 28 kwa wasanii wenye ukwasi zaidi Afrika. Orodha hiyo ilidai kuwa ana ukwasi wa $5 milioni (sawa na Sh. 11,610,000,000 Bilioni).
Diamond alidai hawamfahamu, na kwamba ana fedha nyingi kuliko hizo. Hata hivyo, Forbes walikanusha kutoa orodha hiyo.

Rais Samia Azindua Mfumo Usafirishaji Wa Dharura Kwa Wajawazito Na Watoto Wachanga M-MAMA Jijini Dodoma
Wizkid aonesha ukomavu wa kiushindani