Mkali wa muziki kutoka nchini Nigeria Ayodeji Ibrahim Balogun maarufu Wizkid ametoa pongezi zake za dhati kwa wasanii wenzie kutoka Afrika ambao kwa pamoja walishiriki katika kuwania tuzo za Grammy za 64 zilizotolewa mapema April, 2022.

Wizkid ametuma salama hizo kwa Angelique Kidjo kutoka Benin ambaye ni mshindi wa tuzo katika kipengele alichokuwa akiwania Wizkid na salamu nyingine ni kwa DJ maarufu kutoka Afrika ya kusini Black Coffee.

Wizkid ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram (Insta story) kuwasilisha pongezi hizo, akidhihirisha wazi kuridhishwa na matokeao licha ya kundi kubwa la mashabiki wake kuendelea kupaza sauti zao kuwa msanii huyo ndiye aliyestahili kushinda tuzo hizo.

“Upendo kwa kaka yangu mfalme Black Coffee na Malkia Angelique Kidjo kwa ushindi na kuendelea kuling’arisha bara la Afrika. Muziki wa Afrika unakua.” Ameandika Wizkid.

Kwenye tuzo za Grammy za 64 zilizofanyika mwaka huu, jina la mwanamuziki WizKid lilitajwa katika vipengele viwili ambavo ni Best Glonal Music Album ‘Made in Lagos Deluxe Edition’ pamoja na Best Music Perfomance ‘Essence’.

Forbes yaanika utajiri wa wasanii 2022, Diamond aweka wazi?
Onyango kuikosa Orlando Pirates kwa Mkapa