Mwanamuziki French Montana ametangaza ujio wa Album yake mpya iitwayo “They Got Amnesia” inayotarajiwa kuachiwa rasmi Novemba 12, 2021.

Kupitia album hiyo rapa French Montana ameweka wazi kuwa anataka Dunia itambue aliyoyapitia na namna alivyoupigania Uhai wake akiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), alivyopoteza uwezo wa kukumbuka chochote, Marafiki na watu wengine ambao hakuweza kudhani kama wangetoweka kiasi cha kukosa matumaini ya kuendelea kuishi Duniani.

French Montana anasema baada ya kupoteza kila kitu aligundua kwamba aliyebaki naye ni Mwenyezi Mungu pekee.

Hivyo aliweka matumaini kwake na kumuomba ampe nafasi ya kuendelea kuishi. “Nashukuru kuwa hapa kusimulia hadithi ya maisha yangu. Miaka miwili iliyopita siku kama hiyo nilikuwa ICU nikipigania maisha yangu.

Upotevu wa kumbukumbu, Marafiki waliotawanyika karibu wote, na nilipokuwa chini nikagundua kuwa nilivhokuwa nacho ni Allah pekee, akaniinua na kunipa nafasi ya pili, nilipojaribu kurudi wakanihesabu na kusahau kila tulichofanya Siku ya 730″. Amendika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

“They Got Amnesia itakayotoka Nov 12, 2021”, itakuwa album ya nne kwa French Montana tangu kuingia rasmi kwenye tasnia ya muziki.

Rais Samia kuhutubia Mkutano wa COP 26
Mrithi wa Gomes kutangazwa juma hili