Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC huenda wakamtangaza Kocha Mpya atakayerithi mikoba ya Didier Gomes.

Simba SC iliachana na Gomes mwanzoni kwa juma lililopita, baada ya matokeo mabaya dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Afisa Mtengaji Mkuu Barbara Gonzalez amesema: “Tutampata kocha mkuu mara baada ya mechi na Namungo kisha ataanza kazi wakati ligi imesimama kutokana na ratiba ya timu ya taifa hapo atakuwa na muda wa maandalizi ingawa wachezaji wote hawatakuwepo,”

“Kuna kocha mmoja wa Afrika ameomba kazi na tumeanza kufanyia kazi wasifu wake kama utakuwa vile ambavyo tunahitaji tutafanya nae kazi lakini kuna wengine hawakuomba nao tunawafuatilia,”

“Tunahitaji kocha ambaye hatakuwa na wasifu mkubwa mno kwani atakuwa na malengo ya kupata mafanikio na kuongeza ubora wake kwa kuchukua mataji na kufanya vizuri kupitia Simba.”

French Montana asimulia alivyonusurika Kifo
Masau Bwire: Tunapeleka msiba Jangwani