Polisi nchini Kenya, wamefanikiwa kukamata shehena ya magunia 12 ya bangi, yaliyokuwa yakisafirishwa kupelekwa Kisumu kwa gari la kubebea maiti.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kaunti ya Busia, Maxwell Nyaema amesema gari hilo la Rafiki Funeral Services-Othaya, lilikamatwa baada ya  kusimamishwa kwa ukaguzi wa kawaida.

Amesema, ” sasa dereva aliposhusha dirisha, Afisa wa Polisi aligundua harufu isiyokuwa ya kawaida na baada ya upekuzi waliyaona magunia hayo yamepangwa sehemu ya kuweka jeneza.

Kufuatia tukio hilo, Kamanda Nyaema amesema Polisi haitasita kuwachukulia hatua watu wote wanaoenda kinyume na taratibu au sheria zilizowekwa, huku akiwasihi wahalifu kutafuta njia salama za kujitafutia kipato.

Wananchi wapewe elimu ya Katiba: Dkt. Ndumbaro
Ndege isiyo na Rubani kusaidia makabiliano visumbufu vya Mazao