Afisa Mtendaji Mkuu wa Geita Gold FC Simon Shija amesema kuna uwezekano wa kikosi chao kuwaka Kambi Afrika Kusini kwa ajili ya Kujianda na msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Geita Gold FC itashiriki kwa mara ya kwanza Michuano ya Kimataifa (Kombe la Shirikisho Barani Afrika), kufuatia kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita 2021/22.

Shija amesema wapo kwenye taratibu za kuhakikisha kikosi chao kinapata nafasi ya kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuweka kambi kwa siku kadhaa, huku wakiamini fursa hiyo itawawezesha wachezjai wao kuwa na mazingira mazuri wa kujiandaa Kimataifa.

“Kambi yetu itaanza Julai 20, kwa sasa tupo kwenye mandalizi lakini pia tunaangalia kama kuna uwezekano wa kwenda nje ya nchi kufanya maandalizi ya msimu mpya (Pre-Sesoan), kwa siku chache kwa ajili ya kuwajengea uwezo wachezaji wetu.”

“Lengo la kwenda nje ya nchi ni kuwajenga wachezaji wetu kisaikolojia ili wahisi wapo katika levo ya kupambana kimataifa, tunafikiria kwenda Afrika Kusini ama nchi nyingine yoyote hapa hapa Afrika, lakini bado hatujapata muafaka sahihi.”

Katika hatua nyingine Shija amewataka Mashabiki wa Geita Gold FC kupuuza taarifa za usajili zinaoendelea kuchukua nafasi kwenye Mitandao ya Kijamii, kwani hadi sasa hakuna taarifa rasmi kutoka kwao kama viongozi.

“Kuhusu wachezaji tuliowasajili mpaka sasa zote ni tetesi, muda muafaka ukifika tutasema, kwa ufupi wachezaji wote tuliomaliza nao msimu na Benchi la Ufundi wote wapo, tutaachana na wachezaji wachache ili kutoa nafasi kwa wachezaji wapya kusajiliwa.” amesema Shija

Deus Kaseke ang'olewa Young Africans
Shomari Kapombe atangaza vita mpya Simba SC