Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Klabu ya Young Africans imetangaza kuachana na Kiungo Mshambuliaji Dausi Kaseke, katika usajili wake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa inayoratibiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Kaseke anakua mchezaji wa kwanza kuachwa na Young Africans katika kipindi hiki, ambacho klabu hiyo inaendelea kufanya usajili wa wachezaji wa kimataifa.

Taarifa za kuachwa kwa Kaseke klabuni hapo zimetolewa kwenye kurasa za Mitandao ya Kijamii ya Klabu ya Young Africans.

Taarifa hiyo imeandikwa: ?????? ???? ??????

Umekuwa sehemu kubwa ya mchango wa mafanikio kwenye Klabu yetu, Tunakutakia kila la kheri na mafanikio uendako.

???? ?????????, ?????? ??????????

Kaseke alisajiliwa Young Africans kwa vipindi viwili tofauti, awali alisajiliwa klabuni hapo mwaka 2015 akitokea Mbeya City, mwaka 2017 aliondoka klabuni hapo baada ya kusajiliwa Singida United.

Mwaka 2018 Kaseke alirudishwa Young Africans, ambapo ameitumikia klabu hiyo hadi leo imethibitika anaondoka rasmi.

Okrah atuma ujumbe Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho
Geita Gold FC kufuata yanyo za Simba SC, Young Africans, Azam FC