Hatimaye Klabu ya Geita Gold FC imeanza kufanya usajili kuelekea Michuano ya Kimataifa na Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa kumtangaza Beki wa kulia wa Tanzania Aman George Wawa, akitokea Dodoma Jiji FC.

Geita Gold FC ilikua kimya katika usajili, kufuatia taarifa ya Shirikisho la Soka Duniani ‘FIFA’ kuizuia kwa muda kufanya usajili, kufuatia madai ya yaliyowakabili ya kutomlipa stahiki zake aliyekua Kocha Mkuu Ettiene Ndayiragije.

Kuanza kufanya usajili ndani ya klabu hiyo, ni dhahir zuio la FIFA limeondolewa rasmi na wameanza na Beki huyo wa kulia ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja anakwenda kuongeza nguvu katika eneo la ulinzi wa kulia, akiungana na David Kameta ‘Duchu’ aliyejiunga na timu hiyo msimu uliopita.

Wawa ametambulishwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na kusindikizwa na ujumbe wa kusifia kipaji chake.

“Geita Gold FC tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba na mlinzi wa kulia George Aman Wawa,”

“George Wawa alikuwa akitumikia klabu ya Dodoma Jiji, moja kati ya mafundi wa mpira wenye akili ya ulinzi na mbinu za kisasa. Karibu Geita, Karibu saana kwa wawakilishi wa kimataifa,” imesema taarifa hiyo.

Awali Mtendaji Mkuu wa Geita Gold, Simon Shija alisema walichelewa kutambulisha wachezaji wao kutokana na kuweka sawa masuala ya mikataba na sheria ili kuepuka usumbufu na migogoro inayoibuka baina ya wachezaji na timu.

Mifugo 314 yaingia nchini kinyume cha sheria
Vipers SC yashikilia dili la Manzoki kwa Milioni 450